Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika Taasisi ya Sayansi za bahari Zanzibar


 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Buyu, Zanzibar kujionea maendeleo ya taasisi hiyo na kuongea na jumuiya ya wafanyakazi na wanafunzi.

Mkuu wa Chuo amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa juhudi zinazofanywa za kutafiti, kufundisha na kutoa huduma kwa jamii katika nyanja mbalimbali za kilimo na ufugaji wa kwenye maji. Ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha kuwa chuo kinafikia malengo yake na kusaidia maendeleo ya Taifa.