Tunapenda kuitaarifu Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Umma kwa ujumla kuwa, katika kutimiza wajibu wake kwa Taifa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimewasilisha kwa Serikali gawio la Shilingi Bilioni Moja. Gawio hili liliwasilishwa rasmi kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma mnamo tarehe 8 Januari 2020. Gawio hilo liliwasilishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Mheshimiwa Damian Lubuva(Jaji Mstaafu), Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William A. L. Anangisye na Mwanasheria Mkuu wa Chuo na Katibu wa Baraza Dkt. Saudin Mwakaje.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuboresha maisha ya Watanzania na kupunguza utegemezi kutoka mataifa mengine.

 

Attachment: 20200114_121207_UDSM_KUKABIDHI GAWIO KWA SERIKALI.pdf