Serikali imeazimia kujenga maabara ya muda kwa ajili ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Zanzibar, ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kukidhi mahitaji ya ufundishaji na utafiti wakati utapoanza mwaka wa masomo 2021/22 mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, baada ya maabara iliyokuwepo kuteketea kwa moto.

Maazimio hayo yametolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb.), baada ya kutembelea na kujionea madhara yaliyotokana na ajali ya moto iliyotokea katika jengo la Taasisi hiyo lililokuwa na maabara hiyo lililopo Mizingani, Bandarini, Zanzibar.

SOMA ZAIDI >>>