UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
RESEARCH AND EDUCATION FOR DEMOCRACY IN TANZANIA (REDET)

Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kwa kuzingatia mzunguko wa Uchaguzi, kazi inayofuatia ni kuandaa Taarifa ya Uchaguzi
na kuiwasilisha kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa hii ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, inaelezea kwa undani mchakato wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na namna Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ulivyoendeshwa. Aidha, Taarifa hii inaelezea mafanikio na changamoto zilizojitokeza na mwisho inatoa mapendekezo ili kuboresha chaguzi zijazo.

Taarifa hii ina Sura 11 kama ifuatavyo:-

 1. Utangulizi.
 2. Maandalizi ya Uchaguzi.
 3. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 4. Uteuzi wa Wagombea na Kampeni za Uchaguzi.
 5. Upigaji Kura na Uhesabuji wa Kura Vituoni.
 6. Kujumlisha Kura na Kutangaza Matokeo ya Uchaguzi.
 7. Ushirikishwaji wa Wadau wa Uchaguzi.
 8. Watazamaji wa Uchaguzi.
 9. Tathmini Baada ya Uchaguzi Mkuu.
 10. Mafanikio na Changamoto.
 11. Hitimisho na Mapendekezo.

Ni matumaini yetu kwamba, Taarifa hii itakidhi matarajio ya wasomaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Aidha, Tume inaamini kwamba Wadau wa Uchaguzi, Watafiti na
wasomaji wengine watanufaika na Taarifa hii.

Attachment: Download