UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DIRECTORATE OF PUBLIC SERVICES (DPS)

News

Kurugenzi ya Huduma kwa Umma kupitia kitengo cha Mafunzo Endelevu chatoa mafunzo ya siku tatu kwa wasaidizi wa ofisi kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba,2019.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Dr. Arnold Towo amesema, “wasaidizi wa ofisi hawana budi kufahamu haki na wajibu wa kazi zao kwa kuzingatia kanuni za Utumishi wa Umma”. 

“Kama wasaidizi wa ofisi ni vema kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma muwapo kazini, kufahamu namna bora za utoaji wa huduma kwa mteja pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na kutunza siri za ofisi”, alisema Dr. Towo. 

Pamoja na hayo Dr. Towo aliwasisitiza wasaidizi wa Ofisi kuzingatia Utunzaji wa muda, mali na usalama wa vitu vya ofisi kwa umakini wanapokuwa sehemu zaoza kazi.

Miongoni mwa masuala ya kuzingatia kazini ni kufanyakazi kwa ushirikiano, kutoruhusu migogoro ambayo husababisha msongo wa mawazo, alisema Dr. Towo.

Mafunzo hayo ya wasaidizi wa Ofisi ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi kazini. Mafunzo hayo yatafungwa rasmi tarehe 11 Oktoba, 2019.