UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

CHANGAMOTO

Ni mchezo wa kuigiza wenye vitendo vitatu: katika kitendo cha kwanza tunaonyeshwa walemavu wanakutana na malkia kwenye mlo wa pamoja katika siku ya mwaka mpya. Lengo la mkutano huu ni kuwatia moyo ili wasione ulemavu wao kama kikwazo bali changamoto kaika kujileta maendeleo. Katika kitenso cha pili, tunaoneshwa kadhia waipatayo albino ambapo mganga anatumia Imani za kishrikiana kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi; na kadhia mbalimbali za watu wenye ulemavu zinaonyeshwa . katika kitendo cha tatu tunaona baadhi ya walemavu wanafuata mkondo wa shria ili kutafuta haki zao kama vile elimu, ajira, na upngaji wa mauaji ya albino. Mchezo huu unaishia mahakamani ambako washitakiwa wanaokutwa na hatia wanatumikia adhabu kwa mujibu wa sharia.

Kitabuhiki kitawafaa wanafunzi wa shukw za msingi pamoja na sekondari, hata vyuoni katika somo la fasihi kinafaa vile vilie katika masuala ya kutetea na kusimamia haki za binadamu hasa watu wenye ulemavu.

Tamthiliya hii inatoa changamoto mbalimbali ambazo wanajamii wasio na ulemavu wanapaswa kuzifuata ili kuwatendea haki wenye ulemavu. Upekee wa kazi wa tamthilya hii, unajitokeza katika masuala yaliyodadiliwa humu yaani yanayowahusu watu wenye ulemavu; kwa sababu kazi nyingi za kifasihi hazikuzingatia nafasi yao