UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

FASIHI, LUGHA NA UTAMADUNI WA KISWAHILI NA KIAFRIKA

Ni shahiri na jahara kuwa historia ya fasihi na taaluma za kiswahili haiwezi kuelezwa bila jina la M.M.Mulokozi kutajwa. Kwa hiyo, inatia moyo sana kuona kitabu hichi cha kumuwezi Profesa huyu; hasa kwa vile aghalabu jadi ya kuwaenzi mashujaa wetu, wawe wa kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kijamii kwa jumla, imekuwa ikifadhiwa kwa ajili ya waliotutoka tu.

Inatia moyo Zaidi kuina kuwa wengi wa wachangiaji katika kitabu hiki ni vijana ambao wameamua kushadidia jadi hii ya kuwaenzi watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya lugha hii kuu ya Afrika na fasihi yake. Ari ya kuiona upya Fulani katika Nyanja mbalimbali za lugha na fasihhi ya kiswahili inajutokeza katika kitabu hiki, hasa kuhusu suala la nadharia. Mathalani, kuhusishwa kwa ujumi wa mtu mweusi na pia ubantu kama ilivyofanyika katika sura ya tatu ya kitabu hiki ni dalili tosha kuwa vijana wameanza kusaili, kuchokonoa, kulabizi na kuuliza maswali kuhusu uhalali na ustahiki wa kutimia nadharia ngeni na za nje ya Afrika katika kufanyia tafiti na kuchambukia matokeo ya tafiti hizo za masuala ya Afrika.

Kitabu hiki ni hazina kuu ambayo haitamfanya msomaji amwelewe tu gwiji huyu vizuri Zaidi, bali pia ni buku litakalochochea mijadala ya masuala mbalimbali ya fasihi, lugha na utamaduni wa Kiswahili na kiafrika kaika ngazi mbalimbali shuleni, vyuoni, na kwa wasomaji na watafiti wa kawaida.

(F.E.M.K. Sekoro, Profesa wa Kiswahili, Chuo kikuu cha Namibia, Windihoek, Namibia)

Chapisho hili la kipekee ni mchango maridhawa wa makala za kitaaluma zinazopiga muhuri baraste za kiusomi alizopitia  muashama, mtaalamu na msomi wa Kiswahili, Mugyabuso Mulokozi. Ni Makala zinazocheua fikra pevu za wataalamu waliobobea katika tasnia mbalimbali za bahari kuu ya Kiswahili. Ama kwa hakika, zao hili la kitaaluma bila shaka litamlimbua sio tu limbukeni wa taaluma hii bali pia kumjuza mengi mpenzi shadidi wa Kiswahili.

(Clara momanyi, Profesa wa Kiswahili, Chuo kikuu cha Kikatoloki Afrika mashariki, Kenya)

YALIYOMO:

  1. Profesa Mugyabuso  Mlinzi Mulokozi: Upekee wake kitaaluma na kijamii. (Edith Lyimo)
  2. Mchango wa Mugyabuso Mlinzi Mulokozi katika maendeleo ya fasihi ya watoto nchini Tanzania. (Leonard H. Bakize)
  3. Mchango wa M.M.Mulokozi katika ukuzaji na uendelezaji wa ushairi wa Kiswahili. (Pendo Mwashota)
  4. Ujumi wa mtu mweusi katika kazi za nathari za M.M.Mullkozi. (Shani Omari)
  5. Ujumi wa mtu mweusi katika ushairi wa Kiswahili: mifano kutoka wahairi teule.( Tumaini J. sanga)
  6. Usimulizi katika Nagona na Mzingile: aina na athari zake kwa msomaji. (Rose Jackson Mbijima)
  7. Mbinu za kisanaa zinazosawiri falsafa ya ubuntu katika tamthilia ya tambueni haki zetu. (Anna Nicholaus Kyamba)
  8. Mikondo ya mtiririko wa kishairi: mabadiliko ya ushairi wa Kiswahili wa Kezilahabi na Mulokozi. (Roberto Gaudioso)
  9. Mwingilianomatini katika riwaya za Shaaban Robert: mifano kutoka kusadikika (1951) na kufikirika (1967). (Felix Kwame Sosoo)
  10.  Mtagusano wa kiusemezano kati ya utenzi wa mwana kipona, utenzi wa fumo liyongo na riwaya za siri sirini. (Ombito Elizabeth Khalili)
  11. Uhusiano wa itikadi na mtazamo wa mtunzi: uchunguzi wa riwaya tule za Said Ahamed Mohamed. (Murithi Joseph Jesee, Richard Makhanu Wifula na Kitula Geofyey King’ei)
  12. Mulokozi na suala la ujadi kupitia mazigazi ya Mianzi. (Athumani S. Ponera)
  13. Utambulisho wa mswali: mjadala endelevu uletao changamoto ya kuifasili fasihi ya Kiswahili na utamaduni wa mswahili. (Wallace Mlaga)
  14. Dhana ua maadili katika uandishi wa Shaaban Robert na nafasi yake katika muktadha wa sasa nchini Tanzania. (Adin K. Mutembei)
  15. Matumizi ya istilahi-jadi katika fasihi na jamii kupitia tendi za Kiswahili: mifano kutoka utendi wa Rukiza. (Neema B. Sway)
  16. Ushairi wa Kiswahili kam chombo cha  utetezi wa mwanamke: nwangwi wa jana au uhalisi wa leo? (Clara Momanyi na Joseph Maitaria)
  17. Dhana kanganyifu katika uchapishaji na uchapaji kama msingi wa kuielewa tasnia hiyo. (Timothy T. Mapunda)
  18. Makossa ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya Kiswahili nchini Tanzania. ( Festo N. Joster)
  19. Matatizo ya uandishi katika Kiswahili: maana, chanzo na ufumbuzi. (Titus Mpemba)
  20. Mchango wa viongozi wa Kenya katika kuimarisha lugha ya Kiswahili.(Pamela M. Y. Ngugi)
  21. Mikakati inayotumiwa na vyombo vya habari nchini Kenya kukabiliana na changamoto za Kiswahili. (Stanley Andika Kevogo, Mwenda Mukuthuria na James Omari Ontieri)
  22. Ulinganishi wa kimsamiati baina ya Kiswahili sanifu na kimakunduchi. (Mussa M. Hans)
  23. Michakato mipya ya kueneza dini kiutandawazi na athari zake katika mustakabali kuenea kwa Kiswahili. (Alex Umbima Kevogo, Mwenda Mukuthuria na Ayub Mukhwana)
  24. Uzingativu wa vipengele vya kifani katika kazi za fasihi ya Kiswahili zilizotafsiriwa: mifano kutoka Tamthilia ya Julius Caezar. (Edson Z. Thomas)
  25. Tafsiri katika fasihi ya ulimwengu: mchango, changamoto na mapendekezo . (Hadija Jilala)