UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

JIFUNZE HISABATI

Jifunze  Hisabati  kidato  cha  kwanza  ni kitabu cha Hisabati kwa shule za sekondari  kilichaandikwa  kwa kuzingatia  muhtasari  wa shule za swkondari  nchini  Tanzania.

Ni kitabu cha aina yake kwa kuwa kimetunia lugha ya taifa letu la Tanzania, Kiswahili. Kitabu hiki kimesheheni  istilahi za taaluma ya Hisabati hivyo kukifanya kiwa na ‘ladha’ na mvuto wa pekee. Matumizi ya istilahi za kitaaluma katika kitabu hiki, yanatoa  jibu kwamba “Inawezekana  kufundisha masomo yote, katika viwango vyote vya  elimu nchini kwa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili.”

Mada zimetolewa ufafanuzi wa kina kwa kutumia maelezo kuntu na lugha fasaha. Fauka ya hayo, kitabu hiki kimesheni mifano maridhawa katika kila mada kiasi cha kumfanya mwanafunzi  au mtumiaji aweze kufuatilia na kujifunza Hisabati yeye mwenyewe bila hata msaada wa mwalimu wake.

Kila sura ya kitabu hiki ina mazoezi ya kutosha.  Aidha, baada ya mada ndogo zina mazoezi ya kumsaidia mwanafuzi  katika  yale  anayopaswa kujifunza.  Mazoezi  haya yatampa changamoto mwanafunzi na kufanya ajitume daima hivyo  kujijengea  umahiri  na  ufanisi katika  somo la Hisabati. Vilevile  katika  kurasa  za  mwisho,  kuna  majibu  ya  mazoezi   yote  yaliyomo  kitabuni.  Kujihakiki kama yu sahihi au la.

Kwa kuwa kitabu hiki kimetumia lugha ya Kiswahili ambayo hueleweka vyema  kwa  wengi,  hakuna mashaka  kwamba,  hesabu  zitaeleweka  barabara  na  kupendwa  zaidi.

Dkt. Ernesta S. Mosha,

Mkurugenzi,

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.