UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
INSTITUTE OF KISWAHILI STUDIES (IKS)

Safari ya Chinga

Shani Omari ni Mhadhiri Mwandamizi katika Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.  Chuo kikiuu cha Dar es Salaam. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Kurasini mwaka 1981-1987 na kuendelea katika shule ya sekondari Kibasila mwaka 1988-1991 na baadaye shule ya sekondari ya Zanaki mwaka 1992-1994, zote za mkoa wa Dar es Salaam. Bi Shani Omari ana shahada za BA (Ualimu), MA (Isimu) na PhD. (Fasihi) alizohitimu katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Safari ya chinga ni tamthilia inayoelezea harakati za vijana kutoka vijijini ambao wanakimbilia mijini ili kujikwamua kimaisha. Badala yake maisha hayo yanakumbwa na vikwazo mbalimbali kama vile ukosefu wa kazi za uhakika, kukosa ndugu wa karibu wa kuwasaidia, kukosa mtaji na maeneo rasmi ya kufanyia biashara. Hali hii huwafanya waishi maisha yenye misukosuko na hatima yake ni kitendawili ambacho mteguaji wake inabidi apewe mji.

Kitabu hiki kinafaa kusomwa katika shule za msingi , sekondari, vyuo na jamii kwa ujumla