Hongera Mhe. Dkt. Mpango kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais

Tue, 30.Mar.2021 22.06

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinapenda kutoa pongezi zake za dhati kwa Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Tunajivunia kuwa Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango ni muhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ngazi ya Shahada katika Uchumi 1981-1984, Shahada ya uzamili katika Uchumi 1986-1988 na Shahada ya Uzamivu katika Uchumi 1993-1996.