UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
SCHOOL OF JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION (SJMC)

News

Baraza la Habari Tanzania (MCT) linatarajia kukutana na wanafunzi na walimu wa SJMC kesho Jumanne tar 6 Desemba 2022 hapa shuleni kwetu kuanzia saa 5 hadi saa 7 mchana. Lengo la mkutano huu ni kutaka kuhamasisha umuhimu na utekelezwaji wa AZIMIO LA DAR ES SALAAM JUU YA UHURU WA UHARIRI NA UWAJIBIKAJI (DEFIR).

Pamoja na watendaji wa MCT, pia watakuwepo Profesa Issa Shivji pamoja na Jenerali Ulimwengu ambao ndio wazungumzaji wakuu kuhusu Azimio hili la Dar es Salaam ambalo linaihusu sekta ya habari.