Skip to main content
Body

Salamu za Pole

Mkuu wa Chuo, Baraza, Menejimenti na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Profesa Keto Elitabu Mshigeni kilichotokea tarehe 22 Machi 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipokuwa akipatiwa matibabu.

Profesa Mshigeni alizaliwa tarehe 14 Januari 1944 katika Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Mpinji (1952 – 1955) na baadaye Shule ya Msingi Suji (1958 – 1959), kabla ya kuendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Tabora (1960 – 1965). Alipata elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alihitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi mwaka 1969 kabla ya kuendelea na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Hawaii na kuhitimu mwaka 1974.

Profesa Mshigeni aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1969 kama Mkufunzi Msaidizi na baadaye kupanda ngazi mbalimbali za kitaaluma hadi kufikia hadhi ya Profesa mwaka 1979. Katika kipindi cha utumishi wake chuoni, aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Botania (1976–1982) na baadaye kuwa Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kurugenzi ya Masomo ya Uzamili kuanzia mwaka 1980 hadi 1990. Kupitia nafasi hizi alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha tafiti, kukuza ubora wa masomo ya uzamili na kuendeleza watafiti chipukizi.

Soma Zaidi >

Announcement Date