Body
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 02/05/2026 hadi 04/05/2026 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji anachotoka.
Announcement Date