Vyakula Vyenye Wanga: Vyakula hivi ni pamoja na aina zote za nafaka, viazi aina zote mihogo, magimbi, na Ndizi. Vyakula hivi huupatia mwili nguvu.
Vyakula Vyenye Protini: Aina hii ya vyakula ni pamoja na maharage, kunde, mbaazi, soya, karanga, njegere, njugu mawe, dengu, choroko, asili ya wanyama ni: nyama, mayai, samaki, dagaa, kumbikumbi, senene, maziwa na nzige. Vyakula hivi hujenga mwili.
Vyakula Vyenye Vitamini na Madini: Aina hizi za vyakula ni pamoja na matunda aina zote na mboga-mboga za aina mbalimbali. Vyakula hivi huupa mwili kinga imara dhidi ya maradhi mbalimbali
Vyakula Vyenye Mafuta na Sukari: Aina hii ya vyakula ni pamoja na mafuta ya kupikia, aina zote za ufuta asali, miwa nakadhalika.
Tafadhali bonyeza hapo chini kupakua jarida kwa maelezo zaidi