Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam akikagua miradi na maeneo ya kituo cha utafiti wa bahari Pangani-Tanga


 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akikagua miradi na maeneo ya Kituo cha Utafiti wa Bahari kilichopo Pangani, Tanga. Kituo hicho kiko chini ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS). Katika ziara hiyo Makamu Mkuu wa Chuo aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utawala, Mkurugenzi wa TSB na maafisa wengine wa Chuo. Makamu Mkuu wa Chuo aliahidi kukiboresha kituo hicho kiwe cha kimataifa, kwa kufanyia kazi changamoto za majengo, mahabara, hosteli na mabwawa ya mafunzo ya ufugaji wa samaki.