UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
SCHOOL OF JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION (SJMC)

News

HONGERA KELVIN KANJE KWA KUPOKEA TUZO YA MFANYAKAZI BORA KITAIFA

Uongozi na menejimenti ya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC) unatoa pongezi za dhati kwa Kelvin Kanje kwa kushika nafasi ya kwanza na kupokea tuzo ya Mfanyakazi Bora Kitaifa, iliyotolewa katika Siku ya Wafanyakazi Duniani(Mei Mosi) tarehe 01 Mei, 2023. 
Uongozi wa SJMC unaendelea kujivunia ubora na mafanikio makubwa ya wahitimu wa Shule hiyo Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwemo Kelvin Kanje. 
Kelvin Nicomedius Kanje alidahiriwa Katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC) kama mwanafunzi wa Shahada ya Awali ya Mahusiano kwa Umma, mnamo mwaka 2012 na kuhitimu shahada hiyo mwaka 2015 akiwa na namba ya usajili 2012-04-03245. 
Kelvin Kanje ni Mtaalamu wa masuala ya Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma katika Idara ya Habari – MAELEZO iliyochini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.