UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
SCHOOL OF JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION (SJMC)

News

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC)  tarehe 20 Machi, 2023 kimeendesha mafunzo kwa watumishi ili kuboresha huduma kwa wateja wa chuo hicho. 

Akifungua mafunzo tarehe 20 Machi, 2023 Amidi wa shule hiyo Dkt. Mona Mwakalinga amesema mafunzo hayo ni chachu ya kudumisha uhusiano mwema miongoni mwa watumishi na kati ya watumishi na wateja wa shule hiyo. Amesema kupitia mafunzo hayo yataboresha huduma zinazotolewa na SJMC ambazo pia zinaakisi huduma za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wawezeshaji kutoka katika Kitengo cha Ushauri na Unasihi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamewasilisha mada mbalimbali ikiwemo; Mafunzo ya Huduma kwa Wateja, yaliyowezeshwa na Bw. Antidius Fidelis; Kujenga Motisha ya Kazi na Ushirikiano katika Kazi, mada iliyowasilishwa na Bw. Ally Sanga, na Utatuzi wa Migogoro Mahala pa Kazi, mada iliyowasilishwa na Bw. George Chacha.


Akifunga mafunzo hayo Afisa Tawala, SJMC Bi. Justina Karata amesema ni imani yake kuwa mafunzo hayo yataleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma kwa wateja na zaidi yatajenga uhusiano mwema.