UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
SCHOOL OF JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION (SJMC)

News

Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Mipango, Utawala na Fedha Prof. Bernadeta Killian ametoa wito kwa wasimamizi wa tovuti za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutumia tovuti hizo katika kusambaza habari na matokeo ya tafiti zilizofanywa chuoni hapo badala ya kusubiri matukio.

 

Prof. Killian ameyasema hayo leo tarehe 03 Februari, 2023 wakati akifungua mafunzo maalum ya Uandishi wa Maudhui ya Tovuti kwa watumishi wa Idara, Ndaki, na Shule za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko cha chuo hicho.

“Tubadilike na tuamke katika kusambaza habari kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tusisubiri matukio tutafute taarifa”- amesema Prof. Killian.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko na mtoa mada katika mafunzo hayo Dkt. Dotto Kuhenga amesema mafunzo hayo yamelenga kutoa uelewa kuhusu aina ya tovuti inayohitajika na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kukitangaza hicho kwa umma.

______

Miongoni mwa mada zilizotolewa katika mafunzo hayo zimejumuisha aina ya maudhui yanayohitajika na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam watoa mada wakiwa ni Dkt. Mussa Kissaka na Dkt. Baraka, Uandishi kwaajili ya tovuti: Habari na maelezo ya picha mtoa mada akiwa ni Dkt. Dotto Kuhenga, Uandishi wa maudhi yenye mwelekeo wa kimasoko na Prof. Masele, Uandishi wa maudhui ya mtandaoni na kupakia habari mto mada, Mr Mkwera.  

#MlimaniMediaUpdates